Hosea 14:5-8


5 aNitakuwa kama umande kwa Israeli;
atachanua kama yungiyungi.
Kama mwerezi wa Lebanoni
atashusha mizizi yake chini;

6 bmatawi yake yatatanda.
Fahari yake itakuwa kama mti wa mzeituni,
harufu yake nzuri kama mwerezi wa Lebanoni.

7 cWatu wataishi tena kwenye kivuli chake.
Atastawi kama nafaka.
Atachanua kama mzabibu,
nao umaarufu wake utakuwa
kama divai itokayo Lebanoni.

8 dEe Efraimu, utasema, ‘Mimi nina shughuli gani tena na sanamu?’
Nitamjibu na kumtunza.
Mimi ni kama msunobari wenye majani mabichi;
kuzaa kwako matunda kunatoka kwangu.”

Copyright information for SwhKC